Hatuwezi kumlazimisha kila mwenye kuswali kuamini yale tunayoamini katika haki na ya sawa. Kwa msemo mwingine ni kwamba hatuwezi kumwambia kila mwenye kuswali kwamba asisome al-Faatihah wakati ambapo imamu anasoma Qur-aan kwa sauti ya juu. Kwa sababu maoni haya yanakabiliwa kwa ukali kutoka kwa wale wenye kufuata kibubusa. Ni kitu kinachohitajia mihadhara, mahojiano na tafiti.

Kwa ajili hiyo sisi ni wenye yakini kabisa kwamba wako waongozwaji ambao wanasoma al-Faatihah. Kwa hiyo sisi hatuwaambii wasisome al-Faatihah isipokuwa baada ya ubainifu, kuwasimamishia hoja na kadhalika. Kama ambavo sio Sunnah kwa sisi ambao ni maimamu wa misikiti, ambao Allaah (´Azza wa Jall) amewaongoza juu ya kufuata Sunnah sahihi, kuwalazimisha wale waongozwaji maoni yao, isipokuwa tu lililo juu yetu ni kuwakumbusha, kwa upande wa pili si haki kwa waongozwaji hawa kuwalazimisha maimamu maoni yao na kumfanya imamu kana kwamba yeye ndiye mwenye kuongozwa na wale wenye kuongozwa wao ndio maimamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (586)
  • Imechapishwa: 04/10/2020