Swali: Kutahadharisha juu ya mapote ya leo na kufichua makosa yao pamoja na watu wanaoenda kinyume na misingi na mfumo wa Salaf inazingatiwa kuwa ni kujeruhi na kusifu, Jar wa Ta´diyl?

Jibu: Nimewaelezeni mara nyingi ya kwamba kujeruhi na kusifu, Jarh na Ta´diyl, ni katika elimu inayohusiana na mlolongo wa wapokezi na Hadiyth na ambayo inafanywa na Muhaddithuun tu.

Ama kuhusiana na kuwaraddi wenye kwenda kinyume, hili sio katika Jarh na Ta´diyl. Huku ni kubainisha haki na kuraddi batili. Sio katika kujeruhi na kusifu. Lengo sio kumjeruhi mtu. Lengo ni kubainisha haki tu na kuonyesha kosa la mkoseaji. Lengo sio kumlenga mtu kwa dhati yake mpaka isemwe kuwa ni kujeruhi na kusifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015