Swali: Je, inafaa kuwaombea du´aa ya kurehemewa, msamaha na Pepo Ahl-ul-Bid´ah?
Jibu: Ikiwa ni waislamu na Bid´ah hazijawatokea katika Uislamu wanaombewa. Wanapewa nasaha na wanalingania kuacha Bid´ah. Aidha wanaombewa na waislamu wengine kwa jumla. Wanazingatiwa ni katika watenda madhambi wenye kumwabudu Allaah pekee. Isipokuwa ikiwa kama Bid´ah zao zinapelekea katika shirki na kufuru na kuwatoa katika dini, katika hali hiyo hapa. Mfano wa Bid´ah hizo ni kumwomba asiyekuwa Allaah, kuyaabudia makaburi, kuyajengea makaburi ili yaabudiwe na kutukuzwa. Hizi ni mfano wa Bid´ah za kishirikina.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ad-Durr an-Nadhwiyd (01)
- Imechapishwa: 07/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)