Swali: Baadhi wamefanya kunyamazia baadhi ya makundi ya kiislamu na ya Hizbiyyah ndio mfumo wao na kwamba kufanya hivo ndio hekima na utaratibu huu umekuwa na wafuasi ambao wanaufuata. Ni ipi hukumu ya mfumo huu mpya wa leo?
Jibu: Nachelea kuna kuongeza chumvi katika swali hili. Mimi siamini kuwa mwanachuoni ambaye anaona hivo na khaswa ikiwa mwanachuoni huyo ni Salafiy. Kwa hivyo nachelea kuna kuongeza chumvi katika swali hili. Lakini tukikadiria kuwa lipo basin ni kosa na ni lazima kwa ambaye anasema, kuona na kuweka msingi huo atubu kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Allaah amepambanua ummah huu na akaufadhilisha juu ya nyumati zingine kwa kutokunyamaza, bali kwa kuweka wazi, kubainisha na kupambana jihaad na katika kilele chake kunakuja jambo la kuamrisha mema na kukataza maovu:
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ
“Mmekuwa Ummah bora kabisa ulioteuliwa kwa watu – mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamwamini Allaah.”[1]
Allaah amewalaani wana wa israaiyl kwa ajili ya kuchukua mfumo kama huo wa kunyamaza na kuikubali batili nyuma ya pazia ya hekima. Amesema (Ta´ala):
لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
“Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa israaiyl kupitia ulimi ya Daawuud na ‘Iysaa mwana wa Maryam – hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakivuka mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule miongoni mwenu atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake na hiyo ni imani dhaifu mno.”[3]
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni msingi mkuu katika misingi ya Uislamu. Uislamu hausimami isipokuwa kwa msingi huo na wala ummah haufikii daraja hii kubwa na ubora na kutangulizwa mbele ya nyumati zingine isipokuwa wakisimama kwao. Wakifanya upungufu basi wanastahi hasira za Allaah bali pengine kulaaniwa kama walivyolaaniwa wana wa israaiyl. Ikiwa wana wa israaiyl walistahiki laana kwa sababu hawakuamrishana mema na kukatazana maovu basi sisi ni aula zaidi. Kwa sababu dini yetu ni kubwa zaidi kuliko dini yao. Kwa hivyo tukifanya upungufu katika dini hii na tukaicha basi wataifanyia mchezo watu wa matamanio na wapotofu na tukawanyamazia na tukaita kitendo hicho kuwa ni hekima. Tukifanya hivo tutakuwa tunastahiki ghadhabu za Allaah. Tunamuomba Allaah atukinge kutokana na ghadhabu Zake. Tunamuomba Allaah – kama kweli kuna watu wa sampuli hiyo – basi awaongoze na awape ufahamu wa njia ya haki na pia akawafahamishe kasoro yao kubwa ambayo wametumbikia ndani yake na watoke humo hali ya kuwa ni walinganizi wa haki na wenye kuamrisha mema na kukataza maovu:
فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ
“Basi tangaza wazi yale unayoamrishwa na jitenge mbali na washirikina.”[4]
Vivyo hivyo tangaza wazi yale unayoamrishwa na jitenge mbali na wazushi na wapotou.
[1] 03:110
[2] 05:78
[3] Ahmad (3/10) na Muslim (49).
[4] 15:94
- Muhusika: ´Allaah Rabiy´ Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 15-16
- Imechapishwa: 10/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)