Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

94 – Amekizunguka kila kitu na Yeye yuko juu yake.

MAELEZO

Ujuzi Wake (Tabaarak wa Ta´ala) umekienea kila kitu. Licha ya kwamba yuko juu ya viumbe elimu Yake imekizunguka kila kitu:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ

“Hakika Allaah hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu.”[1]

Elimu Yake kuyazunguka mambo maana yake ni kwamba anajua kila kitu. Vinginevyo Allaah (´Azza wa Jall) yuko juu.

[1]3:5

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 126
  • Imechapishwa: 10/11/2024