Kuwakodishia watu nyumba kwa pesa kubwa na kuchukua sehemu yake bila mkodishiwa kujua

Swali: Mimi ni miongoni mwa wafanyakazi huko Makkah al-Mukarramah. Mahujaji wanapokuja kwangu wakitaka nikodishe nyumba, basi mimi na mmiliki wa nyumba tunakubaliana kuwa atawakodishia kwa mfano kwa 2.000 na mimi niwe na haki ya 300. Je, huku ni kula rushwa?

Jibu: Lazima awajulishe iwapo yeye na mmiliki wamekubaliana, haifai isipokuwa kwa kuwajulisha. Kwa sababu hii ni katika aina ya rushwa. Yeye anawaambia ni kwa 2.000, kumbe si 2.000 bali ni 1.700. Hili halifai. Ni aina ya rushwa. Iwapo anataka halali, basi awaambie kuwa amekubaliana nao kwa 2.000 na kwamba mimi changu ni 300 iwapo mtakubali, na iwapo hamtakubali basi mtalipa tu 1.700 na yeye mmiliki amenikubalia nichukue 300. Iwapo mtakubali ni sawa vinginevyo acheni au awaambie mfano wa hayo. Kwa msemo mwingine ni lazima awabainishie. La sivyo ni khiyana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30117/حكم-اخذ-عمولة-من-مبالغ-تاجير-البيوت
  • Imechapishwa: 12/09/2025