Swali: Ni ipi hukumu ya kuiga wasomaji wa Qur-aan na makhatwib, ikiwa si kwa ajili ya kuwadhihaki, bali kwa sababu ya kuvutiwa na usomaji wao?

Jibu: Kama mtu anawaiga kwa nia ya kujifunza kutokana na usomaji wao, kuboresha usomaji wake na kuiga uzuri wa kisomo chao, hili ni jambo jema na halina tatizo. Lakini kama kuiga huko kunakuwa kwa ajili ya kuwachezea shere, basi hilo ni kufuru. Kufanya ishtihzai kwa Qur-aan ni kufuru na upotofu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1091/تقليد-المقرىين-والخطباء-ما-حكمه
  • Imechapishwa: 15/12/2025