Swali: Katika mji wangu kuna masanamu yanayoabudiwa badala ya Allaah. Je, niyavunje usiku wakati ambapo hakuna yeyote anayeniona…

Jibu: Hapana, haijuzu kufanya hivo. Hakuna mwenye kuyavunja isipokuwa mtawala peke yake. Wajibu wako ni kukataza shirki, wabainishie watu na mshauri mtawala ayaondoshe. Ni mtawala peke yake ndiye mwenye kutakiwa kuyaondosha. Ukiyavunja usiku watakuua mchana na kujenga mazuri zaidi kuliko yaliyokutwa. Lakini hata hivyo hawatoweza kufanya hivo wala kupinzana ikiwa mtawala ndio atayavunja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20%20-%2025%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017