Swali: Je, mtu anazingatiwa kuwa anaficha elimu akiacha kutahadharisha wenye kwenda kinyume na watu wa Bid´ah?

Jibu: Anaacha kufanya hivo kwa sababu ya kuwaogopa watu? Anaacha kutahadharisha shirki au madhambi mengine kwa ajili ya kuwaogopa watu? Ndio, hili linaingia katika kuwa na woga kwa asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall) na ni aina ya shirki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20%20-%2025%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017