Swali: Mtu aliyemwahidi mtu mwingine kitu kisha akavunja ahadi yake. Je, anapata dhambi?

Jibu: Msingi katika ahadi ni kwamba ni wajibu kuzitimiza. Kuvunja ahadi ni miongoni mwa sifa ya wanafiki:

“… wanapoahidi, huvunja.”

Huu ndio msingi. Isipokuwa kwa sababu inayokubalika katika Shari´ah; kama vile kushindwa kutekeleza au kubadilika kwa kile alichoahidiwa. Kwa maana nyingine sababu inayokubalika katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25413/ما-حكم-من-وعد-شخصا-اخر-بشيء-ثم-اخلف
  • Imechapishwa: 09/03/2025