Swali: Mtu avae kikoi mpaka juu kidogo ya mafundo ya miguu au chini ya hapo?

Jibu: Mpaka kwenye mafundo ya miguu.

Swali: Vipi kikifika mpaka kwenye mafundo ya miguu?

Jibu: Haidhuru. Hata hivyo kisishuke chini ya mafundo ya miguu:

“Kilichoko chini ya kongo mbili za miguu katika kikoi ni Motoni.”

Swali: Hata hivyo hapana vibaya kikifika juu kidogo ya kongo za miguu?

Jibu: Akipandisha juu ya mafundo ya miguu anakuwa amejiweka mbali zaidi na shubuha. Apandishe mpaka kwenye nusu ya muundi.

Swali: Kuna upokezi unaosema kwamba hakuna nafasi ya mafundo ya miguu katika kikoi

Jibu: Imepokelewa katika baadhi ya masimulizi. Lakini Swahiyh zaidi ni ule unaosema:

 “Kilichoko chini ya kongo mbili za miguu katika kikoi ni Motoni.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23311/ما-حد-الازار-حتى-لا-يكون-مسبلا
  • Imechapishwa: 25/12/2023