Swali: Kuna kigezo kipi cha kujifananisha na makafiri?

Jibu: Kuvaa ya mtu yakawa kama mavazi yao, mionekano ya mtu ikawa kama mionekano yao. Baadhi ya mavazi yanafanana na ya makafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”[1]

Wanazuoni wanasema kuwa mwenye kujifananisha na makafiri na akaona kuwa nguo zao ndio bora zaidi, amekufuru, na akivaa mavazi yao bila ya kuona ndio bora zaid, basi anapata dhambi.

[1] Ahmad (5114, 5115 na 5667).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 406
  • Imechapishwa: 24/08/2025