Kuuziana dhahabu kwa dhahabu pamoja na nyongeza ya pesa juu

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kubadilisha dhahabu ya kuvaa kwa dhahabu mpya, kisha akalipa tofauti?

Jibu: Haijuzu kufanya hivyo. Ni lazima anunue dhahabu mpya kivyake, kisha auze dhahabu ya zamani au mbovu kivyake. Kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomwambia Bilaal alipomwambia: ”Tumetumia pishi moja ya tende nzuri kununua mapishi mawili ya tende mbovu.” Ndipo Mtume akasema: ”Oooh oooh, hiyo ni ribaa waziwazi.”

Kwa hiyo usifanye hivyo, bali uza kwa dirhamu, kisha nunua mpya kwa dirhamu. Vivyo hivyo anayekuwa na dhahabu mbovu dhidi ya dhahabu nzuri, atauza kwanza dhahabu mbovu ili apate thamani, kisha atanunua dhahabu mpya kwa hiyo thamani. Ama kuuza hii kwa ile pamoja na nyongeza, hapana. Kwa sababu hapo dhahabu inakabiliwa na dhahabu pungufu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dhahabu kwa dhahabu lazima iwe sawa kwa sawa, sawa kwa uzani, sawa kwa kiasi.”

Kwa hiyo ni lazima dhahabu iuzwe kwa dhahabu sawa kwa sawa, uzani kwa uzani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/983/حكم-تبديل-الذهب-بذهب-مع-دفع-الفارق
  • Imechapishwa: 23/12/2025