Swali: Je, dhahabu zilizoandaliwa kwa ajili ya kujipamba zinatolewa zakaah? Afanye nini mwanamke ambaye analazimika kuuza baadhi ya dhahabu zake ili aweze kutoa zakaah yake?
Jibu: Naona kuwa maoni sahihi ni kwamba ni wajibu dhahabu za kujipamba kuzitolea zakaah zinapofikisha kile kiwango cha wajibu kutoa zakaah ambacho ni gramu 85. Pale ambapo dhahabu inapofikisha gramu 85 basi anawajibika kuitolea zakaah yake. Ikiwa yuko na pesa na akaitolea zakaah, hapana vibaya. Akitolewa na mume wake au mmoja katika jamaa zake, hapana vibaya. Ikiwa yote mawili hayawezekani, basi atauza kile kiasi ambacho anatakiwa kutoa zakaah na kutoa zakaah yake.
Baadhi ya watu pengine wakasema kuwa akifanya hivo basi hatimaye dhahabu yake yote itaisha. Si kweli. Wakati dhahabu zake zitapopungua chini ya kile kiwango ambcho ni cha wajibu kutoa zakaah – ijapo imepungua kidogo tu – basi hatowajibika kutoa zakaah. Kwa maana nyingine ni kwamba ni lazima daima atabaki na vito vya kujipamba. Kwa hivyo kwa mujibu wa maoni yenye nguvu ni kwamba ni wajibu kuyatolea zakaah mapambo ya dhahabu na fedha, ni mamoja anayavaa, kuyaazima au kuyakodisha.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/138-139)
- Imechapishwa: 12/07/2026
Swali: Je, dhahabu zilizoandaliwa kwa ajili ya kujipamba zinatolewa zakaah? Afanye nini mwanamke ambaye analazimika kuuza baadhi ya dhahabu zake ili aweze kutoa zakaah yake?
Jibu: Naona kuwa maoni sahihi ni kwamba ni wajibu dhahabu za kujipamba kuzitolea zakaah zinapofikisha kile kiwango cha wajibu kutoa zakaah ambacho ni gramu 85. Pale ambapo dhahabu inapofikisha gramu 85 basi anawajibika kuitolea zakaah yake. Ikiwa yuko na pesa na akaitolea zakaah, hapana vibaya. Akitolewa na mume wake au mmoja katika jamaa zake, hapana vibaya. Ikiwa yote mawili hayawezekani, basi atauza kile kiasi ambacho anatakiwa kutoa zakaah na kutoa zakaah yake.
Baadhi ya watu pengine wakasema kuwa akifanya hivo basi hatimaye dhahabu yake yote itaisha. Si kweli. Wakati dhahabu zake zitapopungua chini ya kile kiwango ambcho ni cha wajibu kutoa zakaah – ijapo imepungua kidogo tu – basi hatowajibika kutoa zakaah. Kwa maana nyingine ni kwamba ni lazima daima atabaki na vito vya kujipamba. Kwa hivyo kwa mujibu wa maoni yenye nguvu ni kwamba ni wajibu kuyatolea zakaah mapambo ya dhahabu na fedha, ni mamoja anayavaa, kuyaazima au kuyakodisha.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/138-139)
Imechapishwa: 12/07/2026
https://firqatunnajia.com/kuuza-vito-vya-mapambo-kwa-ajili-ya-kuvitolea-zakaah/