Kuuza mali ya mtu aliye na dhiki ya kifedha

Swali: Ikiwa mtu ana dhiki ya kifedha – je, mali zake huuziwa?

Jibu: Majaji huangalia na kuhukumu kulingana na hali yake. Ikiwa ana dhiki ya kifedha, basi hapaswi kuzuiliwa, kwani Allaah amesema:

وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ

”Na ikiwa [mdaiwa] ni mwenye hali ngumu, basi [anayedai] angoje mpaka afarijike.”[1]

Lakini ikiwa ana mali inayoweza kutumika kulipa madeni yake, basi atazuiliwa hadi alipe deni alilonalo.

[1] 02:280

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25386/هل-تباع-املاك-المعسر
  • Imechapishwa: 22/04/2025