Kutumia Siwaak muda kidogo kabla ya swalah ni Sunnah?         

Swali: Nimekuona unatumia Siwaak wakati uliposimama kwa ajili ya swalah. Je, imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufanya hivi na khaswa khaswa katika kipindi hichi? Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema kuswaki katika kipindi hichi kunaweza kumfanya mtu akatokwa na damu?

Jibu: Kutumia Siwaak kabla ya kuswali ni Sunnah, kama walivyosema wanachuoni. Wametumia dalili maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Lau nisingeliutia uzito Ummah wangu, basi ningeliwaamrisha watumie Siwaak katika kila swalah.”

Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba Siwaak ikitumiwa karibu na swalah kinywa ndio kinatwaharika vizuri zaidi. Kwa sababu kwa mfano utaswaki kabla ya kuingia msikitini, ule muda wa wewe kuingia msikitini mpaka kuswali kinywa kinaweza kubadilika. Lakini kuswaki muda kidogo tu kabla ya swalah ndio kutwaharika bora zaidi kwa kinywa.

Kuhusu kwamba damu inaweza kutoka, hili ni kweli. Baadhi ya watu fizi zao zinakuwa na maradhi na pindi wanaposwaki tu wanatokwa na damu. Mtu kama huyu asiswaki. Ikiwa anachelea kutokwa na damu na hawezi kuwa na tishu ambayo atajipangusa kwayo damu. Mtu kama huyu tunamwambia atumie Siwaak wakati atapotawadha ili damu iishe. Na pindi atapotaka kuswaki asiswaki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (09)
  • Imechapishwa: 03/05/2020