Kutumia Siwaak kwa mkono wa kushoto

Swali 136: Ziada inayosema:

“Ilikuwa inampendeza kuanza kwa upande wa kulia… ” na ndani yake imetajwa: “… na katika Siwaak yake.”?

Jibu: Maana yake ni kwamba anaanza na upande wa kulia wa mdomo wake na atumie Siwaak kwa mkono wa kushoto.

Swali 137: Je, Siwaak inatumiwa kwa mkono wa kushoto?

Jibu: Ndio, kwa sababu ni katika kuondoa uchafu na taka na ili aanze na sehemu ya kulia ya mdomo wake, hivyo ndivyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 65
  • Imechapishwa: 26/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´