Swali: Vipi tutakusanya kati ya Hadiyth:

“Lau si mimi angelikuwa katika kina cha chini kabisa cha Moto.”

na katazo la kusema “lau”?

Jibu: Inawezekana, kwa kuwa hili linaweza kuwa limetokana na matumizi au makosa ya baadhi ya wapokezi. Inawezekana kuwa ni jambo linalofaa, kwa sababu baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa inafaa wakitolea hoja Hadiyth hii na vilevile:

“Lau si fulani, fulani angeliangamia.”

au

“Lau si fulani, fulani asingefaulu.”

Lakini kinachotakiwa ni kutumia neno “kisha” kwa kuzifanyia kazi dalili zote. Kama ilivyo katika Hadiyth:

“Msiseme ´kama alivyotaka Allaah na akataka fulani, bali semeni ”kama alivyotaka Allaah kisha ataka fulani´.”

Vilevile Hadiyth ya mtu mwenye ukoma na mwenye upara:

“Sina njia leo isipokuwa kwa Allaah kisha kwa wewe.”

Kwa hiyo Sunnah ni kusema “kisha” na hilo ndilo lililo salama zaidi kwa muumini.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31142/كيف-الجمع-بين-ورود-لو-في-بعض-الحديث-مع-النهي-عنها
  • Imechapishwa: 06/10/2025