Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
133 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
إِذَا مَرِضَ العَبْدُ أَوْ سَافَرَ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ مَا كَانَ يَعْمَلُ مُقِيمًا صَحِيحًا
“Pindi mja anapogonjweka au kusafiri, basi ataandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya katika hali ya ukazi na uzima.”[1]
Inatakikana kwa mtu mwenye busara muda wa kuwa yuko na uzima na nafasi apupie kuleta matendo mengi. Hilo ni kwa sababu pale ataposhindwa kutokana na maradhi au shughuli, basi aandikiwe kikamilifu. Kutumia fursa ya uzima na nafasi kwa kufanya matendo mema ili pale utaposhughulishwa navyo kutokana na maradhi au mengineyo uandikiwe ujira kikamilifu.
[1] al-Bukhaariy (2996).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/189)
- Imechapishwa: 09/09/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket