Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila tendo jema ni swadaqah.”[1]

Wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema ni katika mema mtu anapomtembelea mgonjwa amfanye aweze kufurahi na kumwambia uko na afya njema. Ikiwa mambo ni kinyume kwa maradhi yake kumzidi, amwambie uko na afya njema na huku ni mwenye kunuia ana afya nzuri ukilinganisha na ambaye yuko chini yake. Kumfanya mgonjwa akafurahi ni miongoni mwa sababu za kumfanya akapona.

[1] al-Bukhaariy (6021) na Muslim (1005).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/191)