Kutumia filimbi katika mpira na michezo mingine

Swali: Vipi kuhusu kutumia filimbi?

Jibu: Haipendez. Inapaswa kutumia kitu kingine kuashiria kile kinachokusudiwa badala ya filimbi.

Swali: Lakini siyo kwamba filimbi hiyo inachukuliwa kama ´ibaadah, isipokuwa ni kwa sababu sauti yake ina nguvu. Wala si kupiga makofi kwa mikono, bali kwa kutumia kifaa?

Ibn Baaz: Inawezekana, anaweza kuitumia. Lengo ni kuepuka kujifananisha na watu wa kipindi kabla ya kuja Uislamu. Basi akitumia kitu kingine kinachoweza kusimama mahali pake, hiyo ni kujiepusha na mwenendo wa kipindi kabla ya kuja Uislamu. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29414/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85%C2%A0%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D8%AE%D8%AF%D8%A7%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D8%A7%D9%81%D8%B1%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D9%8A%D8%A7%D8%B6%D8%A9-%D9%88%D9%86%D8%AD%D9%88%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 06/08/2025