Swali: Baadhi ya wachezaji huvaa nguo fupi zinazoishia katikati ya paja. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Ni lazima kufunika paja. Wanazuoni wana mitazamo miwili kuhusu paja kama ni sehemu ya uchi kwa upande wa mwanamume au siyo. Sahihi ambayo imethibitishwa na Sunnah ni kwamba paja ni sehemu ya uchi na ni wajibu kufunikwa. Zipo Hadiyth kadhaa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinazojulisha ya kwamba paja ni sehemu ya uchi. Kwah hiyo ni wajibu kwa mchezaji na asiye mchezaji kuvaa nguo inayofunika hadi kwenye goti au zaidi ili kusiwe na sehemu yoyote ya paja hadi goti inayoonekana. Kiwango cha chini kabisa ni kufunika hadi kwenye goti. Kama atashusha zaidi ya hapo kwa kuchukua tahadhari zaidi, basi hiyo ni bora zaidi. Kinachokusudiwa ni kwamba kiwango cha chini kabisa cha uchi wa mwanaume ni kati ya kitovu na goti.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29407/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85%C2%A0%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%84%D8%A8%D8%B3%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B5%D9%8A%D8%B1%D8%A9-%D9%84%D9%84%D8%B1%D9%8A%D8%A7%D8%B6%D9%8A%D9%8A%D9%86
- Imechapishwa: 06/08/2025
Swali: Baadhi ya wachezaji huvaa nguo fupi zinazoishia katikati ya paja. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Ni lazima kufunika paja. Wanazuoni wana mitazamo miwili kuhusu paja kama ni sehemu ya uchi kwa upande wa mwanamume au siyo. Sahihi ambayo imethibitishwa na Sunnah ni kwamba paja ni sehemu ya uchi na ni wajibu kufunikwa. Zipo Hadiyth kadhaa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinazojulisha ya kwamba paja ni sehemu ya uchi. Kwah hiyo ni wajibu kwa mchezaji na asiye mchezaji kuvaa nguo inayofunika hadi kwenye goti au zaidi ili kusiwe na sehemu yoyote ya paja hadi goti inayoonekana. Kiwango cha chini kabisa ni kufunika hadi kwenye goti. Kama atashusha zaidi ya hapo kwa kuchukua tahadhari zaidi, basi hiyo ni bora zaidi. Kinachokusudiwa ni kwamba kiwango cha chini kabisa cha uchi wa mwanaume ni kati ya kitovu na goti.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29407/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85%C2%A0%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%84%D8%A8%D8%B3%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B5%D9%8A%D8%B1%D8%A9-%D9%84%D9%84%D8%B1%D9%8A%D8%A7%D8%B6%D9%8A%D9%8A%D9%86
Imechapishwa: 06/08/2025
https://firqatunnajia.com/bukta-na-kaptula-kwa-wachezaji-mpira/