Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Aayah za Qur-aan nje ya mahali pake, kama vile kumwambia mtu anayeitwa Yuusuf:

يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا

“Yuusuf yapuuzilie mbali haya.”[1]

au kusema:

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ

“Haubakishi wala hauachi kitu.”[2]?

Jibu: Hili halitakikani. Ama kunukuu kutokana na Aayah za Qur-aan, hilo halina ubaya ikiwa kunukuu huko kutakuwa katika mahali pake panapostahiki. Lakini ikiwa ni katika mahali pasipokuwa pake, basi haifai.

[1] 12:29

[2] 74:28

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 12/09/2026