Afupishe swalah anapoenda shambani kwake 400 km?

Swali: Nina shamba lililo umbali wa 400 km kutoka Riyaadh. Huenda huko mara kwa mara na hukaa siku mbili au tatu. Je, inajuzu kwangu kufupisha swalah?

Jibu: Ndiyo. Wewe ni msafiri na hivyo unaruhusiwa kufupisha swalah. Lakini ukisikia adhaana na ukawakuta watu wanaswali kwa mkusanyiko, basi swali pamoja nao na ukamilishe swalah. Ama ukiwa peke yako au ukiwa pamoja na wasafiri wengine, basi fupisha swalah.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 12/09/2026