Wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah wameona juu ya kufasiri Hadityh hizi na mfano wake, ambazo zimetaja waziwazi tamko la kufuru, shirki, kukanusha imani au kujitenga mbali, kama mfano wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Aliyetufanyia ghushi si miongoni mwetu.”
“Pepo ni haramu kwake.”
“Haingii Peponi mbea.”,
wakabainisha kuwa lengo si kumtoa mtenda hayo katika Uislamu, bali makusudio ni onyo kali kwa mwenye kufanya hivo na kwamba anastahiki adhabu hiyo ikiwa atahalalisha tendo hilo, kwa sababu kulihalalisha kunamfanya awe kafiri. Ikiwa si hivyo, basi Allaah ndiye atayeamua cha kumfanya.
- Muhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 462
- Imechapishwa: 11/09/2026
Wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah wameona juu ya kufasiri Hadityh hizi na mfano wake, ambazo zimetaja waziwazi tamko la kufuru, shirki, kukanusha imani au kujitenga mbali, kama mfano wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Aliyetufanyia ghushi si miongoni mwetu.”
“Pepo ni haramu kwake.”
“Haingii Peponi mbea.”,
wakabainisha kuwa lengo si kumtoa mtenda hayo katika Uislamu, bali makusudio ni onyo kali kwa mwenye kufanya hivo na kwamba anastahiki adhabu hiyo ikiwa atahalalisha tendo hilo, kwa sababu kulihalalisha kunamfanya awe kafiri. Ikiwa si hivyo, basi Allaah ndiye atayeamua cha kumfanya.
Muhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 462
Imechapishwa: 11/09/2026
https://firqatunnajia.com/makusudio-ya-hadiyth-hizo-ni-makemeo/