Allaah amesema:

وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

“Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke ikateni mikono yao – ni malipo kwa yale waliyoyachuma, ndio adhabu ya kupigiwa mfano kutoka kwa Allaah. Allaah ni Mwenye nguvu kabisa, Mwenye hekima ya yote.”[1]

Basi lau kuwa mwenye kufanya dhambi kubwa duniani anastahiki kudumu katika Moto, kama hawa makafiri, basi Allaah angeamrisha kukatwa shingo za mwizi wa kiume na wa kike badala ya mikono yao. Kwa sababu haingii kudumu Motoni isipokuwa kafiri au mnafiki wa unafiki kiimani, kwani yeye amemkufuru kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama ilivyotajwa hukumu ya wanafiki katika Aayah zilizotangulia.

Kadhalika aliyeacha dini baada ya Uislamu wake kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote mwenye kubadibadilisha dini yake, basi muueni.”[2]

Mtenda dhambi kubwa hajabadilisha dini yake. Ndio maana Allaah akaamrisha mwizi akatwe mkono, lakini hajahukumu akatwe kichwa chake. Aayah hii na nyinginezo mfano wake zinatosha kuwa ni Radd kwa al-Khaliyliy na wenye kuona maoni yake na kuamini ´Aqiydah yake ambayo inapingana na dalili za Qur-aan na Sunnah Swahiyh.

[1] 05:38

[2] al-Bukhaariy (6922).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 402
  • Imechapishwa: 11/09/2026