´Aqiydah ya az-Zamakhshariy hii ndiyo ´Aqiydah ya mwandishi al-Khaliyliy, nayo ni ´Aqiydah ya Ibaadhiyyah. Hivi ndivyo wanavyomtendea mwenye kutenda dhambi kubwa, ingawa duniani wanamuita kafiri wa neema (كافر نعمة). Hata hivyo huko Aakhirah ni mwenye kuwekwa Motoni milele.

Lakini kunasibisha kwa al-Khaliyliy ´Aqiydah hii kwa Ibn ´Attwiyyah, al-Qurtwubiy na ash-Shawkaaniy ni madai yasiyo sahihi. Tunasikitikia kwa mfano wa al-Khaliyliy – japokuwa si jambo la kushangaza kwake wala kwa mfano wa walioko katika mkondo wake – kwamba ananasibisha kwao kauli na hali haelezi marejeleo wala kitabu alichotoa humo. Pamoja na kwamba vitabu vyao vipo karibu mkononi mwake. Kitendo hiki ni kinyume na misingi ya utafiti wa kielimu.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 377
  • Imechapishwa: 11/09/2026