Ikiwa Ibn Abiy Du-aad na wengineo walishindwa kuwasilisha dalili kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah kumpa al-Mu´taswim – ambaye alikuwa ndiye khaliyfah wa `Abbaasiy – ili ampe Imaam Ahmad bin Hanbal katika ule mjadala, matokeo yake wakageukia kutumia nguvu na ukatili. Basi atapata wapi al-Khaliyliy – ambaye anachochea fitina upya ili kutenganisha umoja wa ummah – dalili kutoka katika ndnai ya Quur-aan na Sunnah juu ya Bid´ah hii ya kusema kuwa ”Qur-aan imeumbwa”?

  • Muhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 354
  • Imechapishwa: 11/09/2026