Kutoka katikati ya Khutbah za kisiasa na kwenda msikiti mwingine

Swali: Siku moja ya Ijumaa nilihudhuria Khutbah kwa Imamu mmoja. Wakati alipoanza Khutbah yake akaanza moja kwa moja kuzungumzia jambo la kisiasa. Nikasimama katikati ya Khutbah na kudhihirisha kuchukia kwangu Khutbah yake na nikaenda Msikiti mwingine. Je, kitendo changu hichi ni sahihi?

Jibu: Ikiwa Khutbah yake haina faida na ukaenda kwa mwingine ili uweze kufaidika, kitendo chake hichi ni kizuri na kinatakikana. Ama ikiwa Khutbah yake ina faida na kheri, lakini amekosea katika sehemu yake, sikiliza na akimaliza baada ya Swalah mkumbushe juu ya kitu hichi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-5-29.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014