Kutoga sikio moja matundu mengi

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoga zaidi ya tundu moja kwenye sikio moja kwa ajili ya kuweka dhahabu?

Jibu: Nachelea kitendo hichi kisiwe ni katika israfu. Mwanamke kuweka sikioni mwake zaidi ya vile ilivyozoeleka kidesturi. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ

“Kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye hawapendi wenye kufanya israfu.”[1]

Ikiwa kidesturi imezoeleka kwamba mwanamke anatoga tundu mbili kwenye sikio moja hakuna neno. Ama ikiwa kidesturi haikuzoeleka hivo basi itakuwa ni katika israfu yenye kusemwa vibaya. Kuna khatari wanawake wakawa ujasiri katika jambo hilo na wakaanza kushindana; mwaka huu akatoga tundu mbili, mwaka wa pili akatoga tundu tatu, nne na hatimaye sikio lote likatogwa. Hili si jambo lisilowezekana. Kwani wanawake huigana.

[1] 07:31

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1039
  • Imechapishwa: 08/03/2019