Swali: Ni ipi hukumu ya kutema ndani ya mji wakati wa matabano?

Jibu: Kuna sampuli mbili ya kutema mate ndani ya maji:

1 – Akatema mate kwa kutaraji kupata baraka ya mate ya yule mtemaji. Hapana shaka kwamba kitendo hichi ni haramu na ni aina fulani ya shirki. Mate ya mtu sio sababu ya baraka wala ponyo. Haijuzu kutafuta baraka kutoka katika mabaki ya yeyote isipokuwa tu mabaki ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kunatafutwa baraka kutoka katika mabaki yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa uhai wake na baada ya kufa kwake, kwa sharti ikithibiti kweli kuwa ni mabaki yake. Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa na saa ndogo ya fedha ambayo amehifadhi nywele za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akiwatibu wagonjwa kwazo. Anapojiliwa na mgonjwa, anazimiminia nywele hizi maji, kisha anazitikisa na kumpa mgonjwa anywe kutoka humo ambapo anapona kwa idhini ya Allaah[1]. Lakini haijuzu kufanya hivo kwa mate, majasho, nguo wala kitu kingine cha asiyekuwa Mtume. Bali hiyo ni haramu na ni aina fulani ya shirki, kwa sababu kila ambaye atakithibitishia kitu sababu isiyokuwa ya Kishari´ah wala ya kihisia, basi amefanya sampuli fulani ya shirki. Katika hali hiyo atakuwa amejifanya yeye mwenyewe kuwa ni mfanya sababu pamoja na Allaah.  Kuthibiti kwa sababu juu ya vitu kunatokana na Shari´ah tu. Kwa hivyo kila ambaye atashikamana na sababu ambayo Allaah hakuifanya kuwa ni sababu, si kihisia wala kwa upande wa Shari´ah, basi amefanya aina fulani ya shirki.

2 – Mtu akatema mate wakati wa kusoma Qur-aan tukufu, kama mfano akasoma al-Faatihah. al-Faatihah ni matabano na ndio aina kiubwa ya matabano anayosomewa mgonjwa. Akasomea al-Faatihah na akatema checheza mate ndani ya maji. Kitendo hicho kimefanywa na baadhi ya Salaf na kimeonyesha kuwa kinanufaisha. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akilala kila usiku alikuwa akikusanya vitanga vyake, akivitemea cheche za mate na akisoma ndani yake: “Qul huwaAllaahu ahad”, “Qul a´udhubi Rabbil-Falaq” na “Qul a´udhubi Rabbin-Naas”.” Kisha anajipangusa navyo mwili wake kadri na anavyoweza. Akianza kwa kichwa chake, uso wake na sehemu ya mbele ya mwili wake. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu.”[2]

[1] al-Bukhaariy (5896).

[2] al-Bukhaariy (5016) na Muslim (2192).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/66-67)
  • Imechapishwa: 25/06/2026