Swali: Katika fatwa iliyotangulia umetaja kwamba ni haramu na shirki kutafuta baraka kutoka kwa yeyote asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa tu matabano ya Qur-aan. Hata hivyo imethibiti kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Wakati mtu anapomlalamikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya jambo fulani, kidonda au akawa na jeraha, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hufanya kwa kidole chake namna hii – Sufyaan akaweka kidole chake cha shahaadah ardhini – kisha akakinyanyua na kusema:
بِاسْمِ اللَّهِ، تُرْبَةُ أَرْضِنَا بِرِيقَةِ بَعْضِنَا ، لِيُشْفَى بِهِ سَقِيمُنَا بِإِذْنِ رَبِّنَا
“Kwa jina la Allaah, mchanga ya ardhi yetu na kwa mate ya baadhi yetu, yanaponyesha mgonjwa wetu, kwa idhini ya Mola wetu.”[1]
Tunaomba utuwekee wazi?
Jibu: Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa kitendo hicho ni maalum kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ardhi ya Madiynah peke yake. Katika hali hiyo hakuna utatizi. Hata hivyo kikosi kikubwa cha wanazuoni hawaonelei hivo. Kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kuwa Hadiyth ni yenye kuenea juu ya mate na ardhi zote, hata hivyo kitendo hicho hakihusiani kitu na kutafuta baraka kutoka kwenye mate. Ni mate yenye kuambatana na matabano na udongo kwa ajili ya kutafuta ponyo na sio kwa ajili ya baraka tu. Jawabu langu katika fatwa iliyotangulia inahusiana na kutafuta baraka kutoka kwenye mate peke yake. Kwa hiyo hakuna cha ajabu kwa sababu sura mbili hizo zinatofautiana.
[1] al-Bukhaariy (5745) na Muslim (2194).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/67-68)
- Imechapishwa: 25/06/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/67-68)
Imechapishwa: 25/06/2026
https://firqatunnajia.com/tofauti-kati-ya-matabano-na-kutafuta-baraka/