76. Mabishano ya watenda madhambi na kuacha swalah za mkusanyiko

5 – Hufanya uovu wakati wa kugombana. Kilichokusudiwa hapa ni mtenda dhambi kufanya uovu dhidi ya haki na kwa mwenye haki ili kumdhulumu mali yake, hesima au damu au kuinusuru ´Aqiydah mbovu au mfumo wa dini uliyozuliwa. Kama wanavofanya watu wa matamanio pindi wanapojadiliana na Ahl-us-Sunnah, katia kila zama na kila pahali, kama ilivyopambanuliwa katika vitabu vya Ruduud na vya mahojiano.

Mtenda ana mbinu nyingi katika mabishano. Anaweza kutumia ushahidi wa uwongo, viapo vya uwongo na kuyapambapamba maneno kwa lengo tu la kutaka kufikia lengo lake, khaswa ikiwa inahusiana na kuyanusuru madhehebu yake ya batili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amezikusanya mbinu zote hizi pale aliposema:

“… na anapogombana, hufanya uovu…”

6 – Kuacha swalah za mkusanyiko katika misikiti katika wakati wa ´Ishaa na Fajr. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna swalah nzito zaidi kwa wanafiki kama Fajr na ´Ishaa. Na laiti wangelijua yanayopatikana ndani yake basi wangeziendea ijapo kwa kutambaa. Nimetamani kumwamrisha muadhini akimu swalah kisha nikamwamrisha mtu awaswalishe watu kisha nichukue mwenge wa moto na kuwachoma wale wasiotoke kwenda kuswali.”[1]

[1] al-Bukhaariy (657).

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 166-167
  • Imechapishwa: 25/06/2026