3 – Khiyana. Nayo ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa, ni mamoja inahusiana na haki ya Allaah au haki za viumbe. Allaah (Ta´ala) amekataza khiyana ndani ya Qur-aan pale aliposema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
”Enyi walioamini! Msimkhaini Allaah na Mtume na wala msikhaini amana zenu na hali nyinyi mnajua.”[1]
Kwa hivyo Allaah ameharamisha kumfanyia khiyana Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kuzipoteza na kuzipuuza zile hukumu zilizowekwa katika Shari´ah. Ni haramu pia kuwafanyia khiyana viumbe katika mali, damu na heshima zao. Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wote wawili wameyakataza yote hayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tekeleza amana kwa yule aliyekuamini, na usimkhaini aliyekukhini.”[2]
4 – Usaliti. Usaliti ni kuvunja mikataba ambayo mtu ameahidi ndani ya mipaka ya Shari´ah. Haijuzu kuvunja mikataba bila ya udhuru unaokubalika katika Shari´ah hata kama ni mikataba na kafiri anayeupiga vita Uislamu. Kwa sababu miongoni mwa tabia za waumini ni kuheshima na kutimiza mikataba, kama ambavo kuvunja mikataba ni katika sifa za makafiri, watenda madhambi na waasi. Dalili ya hilo ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu wanafiki:
”… anapoaminiwa anafanya khiyana… “
[1] 08:27
[2] Abu Daawuud (3534), at-Tirmidhiy (1264) na al-Haakim (2/55). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy (Irwaa’-ul-Ghaliyl (1517)).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 166
- Imechapishwa: 25/06/2026
3 – Khiyana. Nayo ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa, ni mamoja inahusiana na haki ya Allaah au haki za viumbe. Allaah (Ta´ala) amekataza khiyana ndani ya Qur-aan pale aliposema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
”Enyi walioamini! Msimkhaini Allaah na Mtume na wala msikhaini amana zenu na hali nyinyi mnajua.”[1]
Kwa hivyo Allaah ameharamisha kumfanyia khiyana Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kuzipoteza na kuzipuuza zile hukumu zilizowekwa katika Shari´ah. Ni haramu pia kuwafanyia khiyana viumbe katika mali, damu na heshima zao. Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wote wawili wameyakataza yote hayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tekeleza amana kwa yule aliyekuamini, na usimkhaini aliyekukhini.”[2]
4 – Usaliti. Usaliti ni kuvunja mikataba ambayo mtu ameahidi ndani ya mipaka ya Shari´ah. Haijuzu kuvunja mikataba bila ya udhuru unaokubalika katika Shari´ah hata kama ni mikataba na kafiri anayeupiga vita Uislamu. Kwa sababu miongoni mwa tabia za waumini ni kuheshima na kutimiza mikataba, kama ambavo kuvunja mikataba ni katika sifa za makafiri, watenda madhambi na waasi. Dalili ya hilo ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu wanafiki:
”… anapoaminiwa anafanya khiyana… ”
[1] 08:27
[2] Abu Daawuud (3534), at-Tirmidhiy (1264) na al-Haakim (2/55). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy (Irwaa’-ul-Ghaliyl (1517)).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 166
Imechapishwa: 25/06/2026
https://firqatunnajia.com/75-khiyana-na-usaliti/