Unafiki wa kimatendo ni aina nane:
1 – Uwongo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Alama za mnafiki ni tatu; anapoongea anasema uongo, anapoahidi anakhalifu na anapoaminiwa anafanya khiyana.”
“Mambo manne yule anayeyakusanya anakuwa ni mnafiki wa kweli na ambaye atakuwa na sifa yake moja katika mambo hayo basi atakuwa na sifa ya unafiki mpaka atakapoiacha; akiaminiwa hufanya khiyana, akisema anasema uwongo, anapoahidi anavunja ahadi yake na anapogombana hufanya uovu.”[1]
2 – Unafiki mwingine wa kimatendo ambao muislamu anapaswa kujihadhari nao ni kuvunja ahadi. Jambo hilo ni dhambi kubwa ingawa watu wengi wanalichukulia wepesi kutokana na ujinga wa yale unapelekea. Kumetolewa maonyo juu ya sifa hiyo na kwamba ni katika mambo ya watu wasiokuwa na nidhamu na sio mambo ya watekelezaji. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu kuvunja ahadi bila ya udhuru:

Imekuja katika tamko jengine:
“… anapogombana, hufanya uovu…”
Imekuja kwa Muslim:
“… hata kama atafunga, kuswali na kujidai kuwa ni muislamu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (58).
[2] Muslim (59).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 165-166
- Imechapishwa: 25/06/2026
Unafiki wa kimatendo ni aina nane:
1 – Uwongo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Alama za mnafiki ni tatu; anapoongea anasema uongo, anapoahidi anakhalifu na anapoaminiwa anafanya khiyana.”
“Mambo manne yule anayeyakusanya anakuwa ni mnafiki wa kweli na ambaye atakuwa na sifa yake moja katika mambo hayo basi atakuwa na sifa ya unafiki mpaka atakapoiacha; akiaminiwa hufanya khiyana, akisema anasema uwongo, anapoahidi anavunja ahadi yake na anapogombana hufanya uovu.”[1]
2 – Unafiki mwingine wa kimatendo ambao muislamu anapaswa kujihadhari nao ni kuvunja ahadi. Jambo hilo ni dhambi kubwa ingawa watu wengi wanalichukulia wepesi kutokana na ujinga wa yale unapelekea. Kumetolewa maonyo juu ya sifa hiyo na kwamba ni katika mambo ya watu wasiokuwa na nidhamu na sio mambo ya watekelezaji. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu kuvunja ahadi bila ya udhuru:
”Alama za mnafiki ni tatu; anapoongea anasema uongo, anapoahidi anakhalifu na anapoaminiwa anafanya khiyana.”
Imekuja katika tamko jengine:
“… anapogombana, hufanya uovu…”
Imekuja kwa Muslim:
“… hata kama atafunga, kuswali na kujidai kuwa ni muislamu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (58).
[2] Muslim (59).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 165-166
Imechapishwa: 25/06/2026
https://firqatunnajia.com/74-uwongo-na-kuvunja-ahadi/