Unafiki wa kiitikadi ni aina sita:
1 – Kumkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sampuli hii ndio iko wazi na khatari zaidi, kwa sbabu inakadhibisha dini yote aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Ta´ala) amesema:
وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ
“Naapa kwa nyota zinapotua. Hakupotoka swahibu wenu na wala hakukosea. Wala hatamki kwa matamanio yake. Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. Amemfunza mwenye nguvu madhubuti. Mwenye muonekano jamili, muruwa na nguvu na kisha akalingamana sawasawa.”[1]
2 – Kuyachukia baadhi ya yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni khatari kwa sababu baadhi ya waislamu wajinga wanaweza kutumbukia ndani ya aina hii ambapo wakatupilia mbali, wakakanusha au pengine hata akapendelea fikira zingine mbele ya baadhi ya hukumu. Huu ni unafiki mkubwa unaompelekea mwenye nao kudumishwa Motoni milele.
3 – Kuchukia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au baadhi ya yale aliyokuja nayo.
4 – Kuchukia kitu alichokuja nacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu hakiafikiani na hakipendezi kwenye nafsi na matamanio ya kishaytwaan. Haijalishi kitu hata kama atafanya kitu hicho anachokichukia kinachengua Uislamu wake. Kwa mfano kuna mtu ambaye anaswali na kufunga lakini wakati huohuo anachukia kuswali na kufunga kwa sababu anaona vinatia uzito na ugumu, ametoka katika Uislamu.
5 – Kufurahi juu ya kudhoofika na kuporomoka kwa Uislamu. Uislamu ndio dini ya haki ambayo Allaah amewakarimu wale awatakao katika watu na majini. Allaah amewatukuza viumbe na Uislamu ulimwenguni na akawafanya wakaweza kuwa viongozi na kuongoza. Kwa Uislamu akawapa maisha mazuri na yenye kubarikiwa duniani, baada ya kufa na Aakhirah. Allaah amrehemu khaliyfah mwongofu ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:
“Sisi ni watu ambao Allaah ametutukuza kwa Uislamu. Tutapotafuta utukufu kwa njia nyingine basi Allaah atatudhalilisha.”[2]
6 – Kuchukia kushinda kwa Uislamu. Ni jambo linalotambulika vyema kuwa makafiri na wanafiki wote huchukia kushinda kwa Uislamu. Sifa hii wako nayo khaswa wanafiki ambao hupatwa na huzuni, wakahisi vibaya na kupatwa na wasiwasi mkubwa pindi Uislamu unaposhinda, kwa sababu wanachukia Uislamu na waislamu.
[1] 53:1-6
[2] al-Haakim (1/130).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 163-164
- Imechapishwa: 25/06/2026

Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 163-164
Imechapishwa: 25/06/2026
https://firqatunnajia.com/73-mfano-wa-unafiki-wa-kiitikadi/