Kutawadha zaidi ya mara tatu

Swali: Je, mtu akihitaji kuosha zaidi ya mara tatu katika wudhuu´  kunazingatiwa ni kuchupa mipaka?

Jibu: Hapana, hii ni ikiwa ana kitu juu ya kiungo kinachozuia maji, basi kwanza akiondoe kabla ya kuanza kutawadha. Ikiwa kuna tope au kitu kingine, basi anapaswa kukiondoa kwanza. Katika hali hiyo sio kuchupa mipaka. Ni lazima akiondoshe. Kuosha mara tatu ni kwa ajili ya wudhuu´, si kwa ajili ya kuondoa uchafu. Kwa mfano kama kuna unga, vidonda vinavyozuia maji au kitu kingine kama matope kinachozuia maji kufika kwenye ngozi, anapaswa kukiondoa kwanza ili aweze kupata ubora wa kutawadha mara tatu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28676/حكم-الزيادة-على-ثلاث-في-الوضوء
  • Imechapishwa: 23/04/2025