Swali: Vipi kuhusu kusoma Qur-aan kwa zamu?
Jibu: Sijui kama kuna kikwazo kuhusu hilo. Unamaanisha watu wa mkusanyiko?
Mwanafunzi: Ndiyo, kwa mkusanyiko. Huyu anasoma ukurasa, kisha mwingine anasoma ukurasa?
Ibn Baaz: Hakuna shida. Kila anapomaliza kusoma mmoja basi mwingine pia anasoma. Wafanya hivo kwa lengo la kujifundisha kwa pamoja. Ni kama ambavo Mtume alifundishwa na Jibriyl (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam).
Swali: Vipi kuhusu wanaosema kuwa kitendo hicho hakikuthibiti kutoka kwa Salaf?
Jibu: Hapana, hapana vibaya. Salaf walikuwa wakisoma na kujifunza Qur-aan kwa pamoja. Aidha imekuja katika Hadiyth Swahiyh:
“Hawatokusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakikisoma Kitabu cha Allaah na wakikidurusu kati yao, isipokuwa wanateremkiwa na utulivu, rehema huwafunika na Malaika huwazunguka na Allaah huwataja kwa wale walioko Kwake.”[1]
Kujifundisha wakati mwingine kunakuwa kwa kukirudia kile kinachosomwa na wakati mwingine inakuwa kwa mmoja kusoma kisha mwingine pia anasoma.
[1] Ameipokea Muslim, Ahmad na katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1308) ya al-Albaaniy.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28699/ما-حكم-قراءة-القران-الجماعية-بالدور
- Imechapishwa: 23/04/2025
Swali: Vipi kuhusu kusoma Qur-aan kwa zamu?
Jibu: Sijui kama kuna kikwazo kuhusu hilo. Unamaanisha watu wa mkusanyiko?
Mwanafunzi: Ndiyo, kwa mkusanyiko. Huyu anasoma ukurasa, kisha mwingine anasoma ukurasa?
Ibn Baaz: Hakuna shida. Kila anapomaliza kusoma mmoja basi mwingine pia anasoma. Wafanya hivo kwa lengo la kujifundisha kwa pamoja. Ni kama ambavo Mtume alifundishwa na Jibriyl (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam).
Swali: Vipi kuhusu wanaosema kuwa kitendo hicho hakikuthibiti kutoka kwa Salaf?
Jibu: Hapana, hapana vibaya. Salaf walikuwa wakisoma na kujifunza Qur-aan kwa pamoja. Aidha imekuja katika Hadiyth Swahiyh:
“Hawatokusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakikisoma Kitabu cha Allaah na wakikidurusu kati yao, isipokuwa wanateremkiwa na utulivu, rehema huwafunika na Malaika huwazunguka na Allaah huwataja kwa wale walioko Kwake.”[1]
Kujifundisha wakati mwingine kunakuwa kwa kukirudia kile kinachosomwa na wakati mwingine inakuwa kwa mmoja kusoma kisha mwingine pia anasoma.
[1] Ameipokea Muslim, Ahmad na katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1308) ya al-Albaaniy.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28699/ما-حكم-قراءة-القران-الجماعية-بالدور
Imechapishwa: 23/04/2025
https://firqatunnajia.com/kusoma-qur-aan-kwa-zamu-na-kwa-kupokezana/