Kutamka nia ni maoni ya ash-Shaafi´iy?

Swali: Nimesikia kuwa kutamka nia mdomo kabla ya swalah ni maoni ya Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah). Je, ni sahihi?

Jibu: Ndio, wanayanasibisha kwa Imaam ash-Shaafi´iy, lakini hayakuthibiti kwa Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah). Wanayanasibisha kwake, lakini hayakuthibiti kutoka kwake (Rahimahu Allaah). Anafuata Sunnah zaidi na ana elimu zaidi na kuijua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%201%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017