Imekuwa ni jambo la kawaida kati ya watu kujitibu kwa nyama ya wanyama wakali, mafuta ya wanyama wakali na damu ya wanyama wakali, khaswa kutoka kwa mbwa mwitu. Tunatumai utatuweke wazi hukumu ya jambo hilo.
بسم الله الرحمن الرحيم
Ni haramu kwa mtu kutafuta matibabu kwa haramu. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) hakujaalia tiba katika yale aliyoharamisha juu ya waja Wake. Kama kungelikuwa faida katika haramu basi asingewaharamishia. Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jitibisheni na wala msijitibishe kwa haramu.”[1]
Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Allaah hakujaalia shifaa ya ummah huu katika vile alivyowaharamishia.”[2]
Kwa maana nyingine ni kwamba haijuzu kula nyama ya mbwa mwitu na simba mwitu, kutumia mafuta yake wala kunywa damu yake kwa lengo la kutafuta matibabu. Ambaye amefanya hivo basi amemuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tukikadiria kuwa amepona kwa kutumia vitu hivyo, basi huyo ni mtihani kwake. Shifaa haipatikani katika hayo kabisa. Hivyo basi, amche Allaah yule anayemwamini na anaogopa siku ya Hesabu. Namuomba Allaah atukinge sisi na ndugu zetu kutokana na ghadhabu na adhabu Yake.
Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn
1416-08-13
[1] Abu Daawuud (3874).
[2] al-Bayhaqiy (10/5).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/55)
- Imechapishwa: 14/07/2026
Imekuwa ni jambo la kawaida kati ya watu kujitibu kwa nyama ya wanyama wakali, mafuta ya wanyama wakali na damu ya wanyama wakali, khaswa kutoka kwa mbwa mwitu. Tunatumai utatuweke wazi hukumu ya jambo hilo.
بسم الله الرحمن الرحيم
Ni haramu kwa mtu kutafuta matibabu kwa haramu. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) hakujaalia tiba katika yale aliyoharamisha juu ya waja Wake. Kama kungelikuwa faida katika haramu basi asingewaharamishia. Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jitibisheni na wala msijitibishe kwa haramu.”[1]
Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Allaah hakujaalia shifaa ya ummah huu katika vile alivyowaharamishia.”[2]
Kwa maana nyingine ni kwamba haijuzu kula nyama ya mbwa mwitu na simba mwitu, kutumia mafuta yake wala kunywa damu yake kwa lengo la kutafuta matibabu. Ambaye amefanya hivo basi amemuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tukikadiria kuwa amepona kwa kutumia vitu hivyo, basi huyo ni mtihani kwake. Shifaa haipatikani katika hayo kabisa. Hivyo basi, amche Allaah yule anayemwamini na anaogopa siku ya Hesabu. Namuomba Allaah atukinge sisi na ndugu zetu kutokana na ghadhabu na adhabu Yake.
Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn
1416-08-13
[1] Abu Daawuud (3874).
[2] al-Bayhaqiy (10/5).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/55)
Imechapishwa: 14/07/2026
https://firqatunnajia.com/kutafuta-matibabu-kutoka-kwa-wanyama-wakali/