Kutafuta baraka kwa maji ya wudhuu´ wa asiyekuwa Mtume

Swali: Je, inafaa kutafuta baraka kwa maji ya wudhuu´ yasiyokuwa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hakutumiwi yeye kipimo kwa wengine, hili ni jambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu hiyo Maswahabah hawakufanya hivyo kwa Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan wala ´Aliy, ingawa wao ndio watu bora zaidi baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili lilikuwa maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam, kwa sababu Allaah ameweka baraka ndani yake. Isitoshe yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwakataza kutokana na shirki na hawakubalii jambo hilo. Ingelikuwa kitendo hicho hakifai, basi asingeliwakubalia kufanya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24686/هل-يجوز-التبرك-بوضوء-غير-النبي-ﷺ
  • Imechapishwa: 26/11/2024