Kuswali Tarawiyh kwa nia ya ´Ishaa

Swali: Mimi nimeswali Tarawiyh pamoja na Imamu lakini kwa nia ya ´Ishaa. Kisha baada ya hapo nikasimama na kurudi kuswali ´Ishaa. Je, kitendo hichi ni sahihi?

Jibu: Vipi utaiswali kwa nia ya ´Ishaa kisha unairudi kuiswali tena? Umeshaswali ´Ishaa inatosha. Inajuzu kuingia na Imamu katika Swalah ya Tarawiyh. Wakati atapotoa Salaam unasimama na kukamilisha Swalah yako. Inajuzu mwenye kuswali faradhi kuongozwa na anayeswali Naafilah. Hakuna haja ya kuirudi kwa kuwa Swalah yako ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (32) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-10-17.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014