Swali: Je, kuna tatizo mtu akaswali swalah ya kupatwa kwa jua au mwezi peke yake?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa mtu ataswali peke yake. Lakini kilichowekwa katika Shari´ah ni kuswali na watu mkusanyiko misikitini. Hili ndio limewekwa katika Shari´ah. Wanawake pia wanatakiwa kuswali pamoja na watu. Hata hivyo hapana vibaya ikiwa wanawake wanaswali majumbani mwao.

Swali: Na vipi kuhusu swala ya ‘Iyd?

Jibu: Ndio, aiswali kwa mujibu wa sifa yake. Lakini ni lazima kuswali ´Iyd pamoja na watu akiweza. Ama ikiwa ni mgonjwa, hapana vibaya ataswali nyumbani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25123/حكم-صلاة-الكسوف-والعيد-منفردا
  • Imechapishwa: 04/02/2025