Ibn Baaz akijibu maswali muhimu kuhusu swalah ya kupatwa kwa jua

Swali: Ni ipi hukumu ya Rukuu´ ya swalah ya kupatwa kwa jua? Ni lini inawahiwa Rak´ah yake? Je, swalah inapaswa kurudiwa ikiwa kupatwa hakukuisha?

Jibu: Sunnah ni kutosheka na swalah moja na isirudiwe. Hata hivyo watu wanashauriwa kujishughulisha na Takbiyr, du´aa, Dhikr na kutoa swadaqah. Swalah ya kupatwa kwa jua haitakiwi kurudiwa. Sunnah ni kusoma Qur-aan mara mbili kwa kila Rak´ah, kufanya Rukuu´ mara mbili na kusujudu mara mbili, huku akirefusha swalah. Hili ndilo lenye usahihi zaidi lililopokelewa kuhusu swalah ya kupatwa kwa jua. Rak´ah mbili inategemea Rukuu´ ya kwanza; mwenye kukosa Rukuu´ ya kwanza, basi amepitwa na Rak´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25126/حكم-ركوعي-صلاة-الكسوف-وتكرارها-اذا-لم-ينكشف
  • Imechapishwa: 04/02/2025