Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
8 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwangu akasema: “Mna chochote?” Nikasema: “Hapana.” Ndipo akasema: “Basi mimi nimefunga.” Akaja siku nyingine kwangu nikasema: “Nimepata tende ya kusagwasagwa.” Akasema: “Nionyeshe nayo. Nilikuwa nimefunga.” Baadaye akaila.”[1]
Ameipokea Muslim.
Hadiyth ni dalili inayoonyesha kuwa swawm ya Sunnah haihitaji nia kuwekwa usiku kabla ya alfajiri, bali inafaa kuweka nia wakati wa mchana. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mna chochote?” Nikasema: “Hapana.” Ndipo akasema: “Basi mimi nimefunga.”
Udhahiri wake ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alianzisha swawm wakati huo, kama inavyoonyeshwa upokezi wa al-Bayhaqiy unaokuja. Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni na pia ni maoni ya baadhi ya Maswahabah, akiwemo ´Aliy na Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ´anhum). al-Bukhaariy amenakili maoni hayo pia kutoka kwa Abud-Dardaa´, Abu Twalhah, Abu Hurayrah, Ibn ´Abbaas na Hudhayfah. Bali Ibn Hazm amepokea kutoka kwa Maswahabah kumi (Radhiya Allaahu ´anhum)[2]. Isitoshe ni maoni ya Abu Haniyfah, ash-Shaafi’iy, Ahmad na wengi katika Salaf[3].
[1] Muslim (1154).
[2] “al-Muhallaa” (06/172).
[3] “al-Istidhkaar” (10/35), “al-Muhallaa” (06/170), “al-Majmuu’” (06/292). Inashangaza kwamba Ibn Hazm haoni kufaa funga swawm ya sunnah kuanzia wakati wa mchana, ijapokuwa amepokea Hadiyth ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na imepokelewa na makumi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), kama ilivyotangulia.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/22-23)
- Imechapishwa: 04/02/2025
Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
8 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwangu akasema: “Mna chochote?” Nikasema: “Hapana.” Ndipo akasema: “Basi mimi nimefunga.” Akaja siku nyingine kwangu nikasema: “Nimepata tende ya kusagwasagwa.” Akasema: “Nionyeshe nayo. Nilikuwa nimefunga.” Baadaye akaila.”[1]
Ameipokea Muslim.
Hadiyth ni dalili inayoonyesha kuwa swawm ya Sunnah haihitaji nia kuwekwa usiku kabla ya alfajiri, bali inafaa kuweka nia wakati wa mchana. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mna chochote?” Nikasema: “Hapana.” Ndipo akasema: “Basi mimi nimefunga.”
Udhahiri wake ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alianzisha swawm wakati huo, kama inavyoonyeshwa upokezi wa al-Bayhaqiy unaokuja. Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni na pia ni maoni ya baadhi ya Maswahabah, akiwemo ´Aliy na Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ´anhum). al-Bukhaariy amenakili maoni hayo pia kutoka kwa Abud-Dardaa´, Abu Twalhah, Abu Hurayrah, Ibn ´Abbaas na Hudhayfah. Bali Ibn Hazm amepokea kutoka kwa Maswahabah kumi (Radhiya Allaahu ´anhum)[2]. Isitoshe ni maoni ya Abu Haniyfah, ash-Shaafi’iy, Ahmad na wengi katika Salaf[3].
[1] Muslim (1154).
[2] “al-Muhallaa” (06/172).
[3] “al-Istidhkaar” (10/35), “al-Muhallaa” (06/170), “al-Majmuu’” (06/292). Inashangaza kwamba Ibn Hazm haoni kufaa funga swawm ya sunnah kuanzia wakati wa mchana, ijapokuwa amepokea Hadiyth ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na imepokelewa na makumi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), kama ilivyotangulia.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/22-23)
Imechapishwa: 04/02/2025
https://firqatunnajia.com/15-hadiyth-basi-mimi-nimefunga/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)