Kuswali nyuma ya anayepinga Hadiyth Swahiyh

Swali: Ni ipi hukumu ya wenye kupinga Hadiyth Swahiyh ambazo zimepokelewa katika al-Bukhaariy na Muslim kama mfano wa Hadiyth zenye kuhusu adhabu ya kaburi na neema zake, Mi´raaj, uchawi, uombezi na kutoka Motoni? Je, mtu aswali nyuma yao, kuwatolea na kuitikia Salaam au mtu awasuse?

Jibu: Wanachuoni wafanye utafiti pamoja na wao kuhusu Hadiyth hizo ili wawafahamishe usahihi wazo na maana yake. Baada ya hapo wakiendelea kuzipinga au kupotosha maandiko yazo kutoka katika maana sahihi kwa kufuata matamanio yao na kufuata maoni yao batili ni watenda madhambi makubwa (mafusaki). Ni wajibu kuwakata na kutochanganyika pamoja nao ili kuepuka shari yao. Isipokuwa ikiwa kuchanganyika pamoja nao ni kwa ajili ya kuwanasihi na kuwaelekeza.

Kuhusu kuswali nyuma yao hukumu yake ni kama hukumu ya kuswali nyuma ya mtenda dhambi. Lililo salama zaidi ni mtu kutoswali nyuma yao. Kwa sababu baadhi ya wanachuoni wamewakufurisha.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/36)
  • Imechapishwa: 24/08/2020