Kuswali makaburini kwa kuchelea kutoka nje wakati wa swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali makaburini pindi mtu anapochelea kumalizika kwa wakati wa swalah?

Jibu: Kuswali makaburini ni batili na swalah haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah awalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu ya kuswalia. Zindukeni! Msiyafanye makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Hakika mimi nakukatazeni kutokamana na hilo.”

Katika Hadiyth nyingine imekuja:

“Ardhi yote ni mahali pa kuswalia; isipokuwa makaburini na vyooni.”

Hii ni Hadiyth ambayo cheni ya wapokezi wake haina neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 21/08/2020