2808 – Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika baada yenu atajitokeza mwongo na mpotoshaji ambaye atasema: “Mmi ndiye Mola wenu.” Yule mwenye kusema: “Wewe siye Mola wetu, lakini Mola wetu ni Allaah, Kwake ndio tunategemea na Kwake ndio tunarejea. Tunamwomba Allaah ulinzi kutokamana na shirki”, basi hatokuwa na utawala juu yake.”

Ameipokea Imaam Ahmad (5/372): Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Ayyuub, kutoka kwa Abu Qilaabah.

Hadiyth ni dalili ya wazi kabisa kwamba yule ad-Dajjaal mkubwa ni mtu mwenye kichwa na nywele timtim. Kwa msemo mwingine ni kwamba sio kinaya cha maharibifu, kama wanavyofikiria watu wenye imani dhaifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/2/727)
  • Imechapishwa: 21/08/2020