Kuswali kwenye msikiti ambao ua wake una kaburi

Swali: Je, inajuzu kuswali kwenye msikiti ambao ua wake una kaburi?

Jibu: Kinachodhiri ni kwamba linapaswa kutolewa ndani ya ua wa msikiti. Hilo ndio wajibu. Likiendelea kubakia namna hiyo, basi hakuna tofauti kati ya swalah inayoswaliwa nje na ndani ya ua wa msikiti – kwa sababu maeneo yote bado ni msikiti. Je, hauna ukuta pamoja na mlango? Kwa hivyo suluhisho kali ni kujenga ukuta unaotenganisha kaburi kutokana na msikiti. Hilo ndio suluhisho. Sioni kuwa ni fikira nzuri kulifukua kaburi na kulihamisha maeneo mengine na pengine ameshakuwa mifupa na takataka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´abr-al-Haatif was-Sayyaarah (2)
  • Imechapishwa: 10/12/2024