Kuswali kabla ya kuingia wakati

Swali: Ni ipi hukumu mtu akiswali kabla ya kuingia wakati?

Jibu: Swalah haisihi mtu akiswali kabla ya kuingia wakati, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]

Isitoshe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha nyakati hizi na kusema:

“Wakati wa Dhuhr ni pale jua litapopondoka.”

Kwa hiyo anayeswali kabla ya kuingia wakati swalah yake haisihi kutokana na faradhi. Lakini inageuka swalah inayopendeza. Kwa msemo mwingine analipwa thawabu kama swalah inayopendeza. Atalazimika kuirudia swalah hiyo baada kuingia kwa wakati.

[1] 04:103

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/215)
  • Imechapishwa: 03/05/2026